VIONGOZI BONDE LA UFA WAPUUZILIA MBALI RIPOTI YA NCIC KUHUSU HALI YA USALAMA ENEO HILO.


Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang amekosoa ripoti ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC iliyotaja kaunti 23 kuwa maeneo ambayo yako katika hatari ya kukumbwa na vurugu katika uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Akizungumza mjini Kitale katika kaunti ya Trans nzoia, gavana Sang ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya viongozi wa eneo la bonde la ufa, amedai kuwa ripoti hiyo ni mojawapo ya mbinu ambazo zinatumika na seriokali kuwazuia wapiga kura kujitokeza kwa wingi ili kushiriki uchaguzi.
Aidha Sang ametumia fursa hiyo kuisuta manifesto ya chama cha azimio akidai kuwa yalkiyomo hayakuhusisha maoni ya wananchi jinsi muungano wa Kenya kwanza unavyokusudia kufanya.