VIONGOZI BARINGO WATAKA USALAMA KUIMARISHWA ENEO HILO.


Viongozi kwenye kaunti ya Baringo wanaitaka serikali ya kitaifa kuimarisha usalama kwenye maeneo ambayo yamekuwa yakishuhudia utovu wa usalama katika siku za hivi karibuni.
Wakiongozwa na mwakilishi akina mama Gladwel Cheruiyot, viongozi hao wamesema kuwa mamia ya wakazi hasa kwenye eneo bunge la Baringo kaskazini kwa sasa wamekimbia makazi yao kutokana na hofu ya kushambuliwa.
Wakiongea katika eneo la kapkiama viongozi hao wameitaka serikali ya kitaifa kushirikiana na ile ya kaunti ili kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na visa vya uvamizi na wizi wa mifugo.
Wamesisitiza kwamba ni wajibu wa serikali kuu kupitia idara zake za kiusalama kuwahakikishia wakenya kwenye maeneo yote ya taifa hili usalama wao na pia wa mali yao.