VIONGOZI BARINGO WASHINIKIZA KUBADILISHEA MBINU ZA KUKABILI UTOVU WA USALAMA KAUNTI HIYO.


Pana haja ya kubadilishwa mbinu za kukabili utovu wa usalama unaochangiwa na uvamizi pamoja na wizi wa mifugo kwenye eneo bunge la baringo kaskazini na kusini kwenye kaunti ya baringo.
Kulingana na Rebecca lomong ambaye ni mmoja wa wawaniaji wa wadhifa wa uwakilishi akina mama kwenye kaunti ya baringo mbinu za awali kama vile kuandaliwa mikutano ya amani imefeli kuzaa matunda.
Lomong’ aidha amewaonya viongozi dhidi ya kutumia swala la utovu wa usalama kujitafutia umaarufu wa kisiasa au kulenga kuchaguliwa kushikilia wadhifa fulani wa uongozi.
Wakati uo huo lomong’ amewashauri akina mama kujitokeza na kuhusika katika harakati za kuhubiri amani na pia kusaka suluhu ya kudumu kwa tattizo la wizi wa mifugo.