VIJANA WATAKIWA KUZINGATIA AMANI MBELE YA UCHAGUZI MKUU UJAO.
Spika wa bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi Catherine Mukenyang’ ametoa wito kwa vijana na jamii ya kalenjin kutoka eneo la Rift valley kufanya siasa za amani wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akihutubu kwenye hafla moja eneo la Talau, Mukenyang’ amesema jamii ya Kalenjin imejulikana kama jamii tulivu na inayopenda amani hivyo inapaswa kudumisha tamaduni hiyo ya tangu jadi.
Aidha Mukenyang’ ametoa wito kwa wakilishi wadi waliomutimua afisini majuma kadhaa yaliopita kufuata sheria baada yake kuelekea mahakamani kupinga hatua ya wakilishi wadi kumtimua afisini kama Spika wa bunge hilo.