VIJANA WATAKIWA KUTOTUMIKA NA WANASIASA MSIMU HUU WA UCHAGUZI.

Vijana katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutokubali kutumika visivyo na wanasiasa kuvuruga amani hasa wakati huu wa siasa za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Ni wito ambao umetolewa na Joseph Limasia kutoaka kacheliba ambaye amewataka vijana badala yake kutumia muda wao kujihusisha na maswala ambayo yatawanufaisha maishani kwani hamna jambo geni katika siasa za mwaka huu.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na Sarich Joseph ambaye amewataka vijana kutochukulia uchaguzi wa mwezi agosti kuwa swala la kufa kupona kwani ni shughuli ambayo itaandaliwa kwa siku moja na kisha kupita.