VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA NA VYUO ANUWAI ILI KUPATA UJUZI WA KUJIAJIRI.


Mwakilishi wadi ya Statunga eneo bunge la Cherangani Kaunti ya Trans Dkt Daniel Kaburu amewahimiza vijana waliokamilisha masomo ya shule za upili na wale waliokosa karo ya kuendeleza masomo yao kujiunga na vyuo vya anuwai ilikujipatia ujuzi wa kiufundi na kujiajiri wenyewe.
Akihutubu eneo la Sinyereri Scheme kwenye wadi yake alipotoa ufadhili wa hema na viti kwa makundi ya akina Mama na vijana eneo hilo, Dkt Kaburu amesema hatua hiyo itasadia katika kukabili ukosefu wa kaziB unaoshuhudiwa kwa sasa kote nchini.
Wakati huo huo Dkt Kaburu ameghadhabishwa na hatua ya mahakama kuu ya kutupilia mbali kwa msada wa marekebisho ya katiba kupitia kwa mchakato wa BBI akisema iwapo ingepasishwa serikali za Kaunti zinge faidi fedha zaidi.