VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI ILIKUJISAJILI KAMA WAPIGA KURA TRANSNZOIA
Huku tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini iebc ikianza zoezi la kuwasajili wa wapiga kura kote nchini hii leo
Mbunge wa kaunti ya transnzoia Bi Janet Nagambo amewarai wakaazi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo iliwasajiliwe kama wapiga kura kama njia moja wapo itakayowapa uhuru wa kuwachagua viongozi wanaowapenda kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea kwenye hafla moja eneobunge la sabaoti amedai baadhi ya wakaazi wameshindwa kufanya maamuzi yao kidemocrasia kwa kuwachagua viongozi wanaopenda
Bi nangabo vilevile ameshtumu baadhi ya viongozi ambao wanagawana nyadhifa za uongozi akidai viongozi wanastahili kuinua maisha ya wakaazi