VIJANA WASHAURIWA KUTOTUMIWA NA WANASIASA ILI KUZUA VURUGU KAUNTI YA BARINGO


Vijana katika kaunti ya Baringo wameshauriwa kutokubali kutumiwa na wanasiasa ili kuzua vurugu taifa linapojiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022.

Akiongea kwenye eneo bunge la Eldama Ravine mwanasiasa Susan Chesaina amesema kuwa vijana hushawishiwa haraka na wanasiasa ambao huwatumia ili kuendeleza malengo yao ya kibinafsi.

Chesaina ambaye analenga kuwania wadhifa wa uwakilishi akina mama kaunti hiyo aidha amewahimiza wakenya kuliombea taifa ili uchaguzi ujao uandaliwe kwa njia ya amani.