VIJANA WAPIGWA JEKI KUPITIA UZINDUZI WA KITUO CHA ICT ENDEBES.

Mbunge wa Endebess kaunti ya Trans nzoia Dkt Robert Pukose amezindua rasmi kituo cha kutoa huduma za mtandao ICT eneo bunge hilo ili kuwasaidia vijana na wenyeji eneo hilo kufanya shughuli za utandawazi.

Akihutubu wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Pukose ametoa changamoto kwa vijana kutumia vyema vifaa akiahidi upanuzi zaidi wa kituo hicho ili kuhudumia vijana na wenyeji wengi zaidi,ikizingatiwa kuwa huduma nyingi za serikali kwa sasa zinatolewa  kupitia njia ya mtandao.

Wakati uo huo Pukose ameahidi ujenzi wa kituo cha kurekodi muziki kwa vijana walio na talanta ya uimbaji akisema hii itakuwa njia moja ya kuwapunguzia wenyeji gharama ya juu ya kurekodi nyimbo zao mbali na kukuza vipaji miongoni mwa vijana.