VIJANA WAONYWA DHIDI YA KUZUA VURUGU KATIKA MIKUTANO YA KISIASA.


Vijana katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua vurugu katika mikutano ya kisiasa ambayo inaendelezwa na viongozi mbali mbali wa siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
OCPD wa Kapenguria Kipkemoi Kirui badala yake amewataka vijana kujihusisha na maswala ambayo yatawanufaisha maishani na iwapo ni lazima wahudhurie mikutano ya siasa basi wasikilize sera za viongozi hao kwa amani na mwishowe kufanya uamuzi wao wenyewe.
Wakati uo huo Kirui amewataka wanasia kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu ujao kwa amani huku akionya kuwa hatua za sheria zitachukuliwa dhidi ya mwanasiasa yeyote atakayepatikana kuhusika na kueneza chuki miongoni mwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi.