VIJANA TRANS NZOIA WATAKIWA KUTOKUBALI KUTUMIA VISIVYO KISIASA.

NA BENSON ASWANI
Wito umetolewa kwa vijana kaunti ya Trans nzoia na taifa kwa jumla kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa kuzua vurugu na badala yake kukumbatia amani.
Akizungumza kwenye hamasisho kwa vijana eneo bunge la Cherangani, mgombea kiti cha mwakilishi kina Mama katika Kaunti hiyo Eunice Karanja, amewahimiza vijana kuwachagua viongozi wanaozingatia amani na watakaohakikisha maendeleo yanaafikiwa ili kuimarisha uchumi wa vijana.
Wakati huo huo Karanja amesema ipo haja ya hamasisho kwa vijana kuhusu usimamizi na uongozi bora mbali na haja ya vijana kuhusika kikamilifu katika mchakao mzima wa uchaguzi ili kuwateua viongozi watakaotilia maanani masilahi vijana.