VIJANA TRANS NZOIA WALALAMIKIA UGUMU WA KUPATA VITAMBULISHO.


Wakazi wa mtaa wa khaluengekaunti ya Trans nzoia wamelalamikia ukosefu wa vitabulisho zaidi ya vijana 500 wakikosa stakabadhi hizo muhimu.
Wakazi hao wanadai hatua zao kutaka kupewa stakabadhi hizo zimegonga mwamba kutokana na ukosefu wa fedha za usafiri pamoja na vigezo vingi vimepelekea hali hio.
Si vijana tuu kwani hata wazee waliopoteza stakabadhi hizo wameshindwa kuzipata tetesi za mapendeleo zikiibuliwa.