VIJANA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUTOKUBALI KUTUMIKA VISIVYO NA WANASIASA.


Vijana wametakiwa kukumbatia amani na kukataa kutumika na wanasiasa katika kuvuruga mikutano ya wapinzani wao msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Ni wito wake msimamizi wa wadi ya Lomut katika kaunti hii ya Pokot magharibi Meshack Lotuliang’iro ambaye amesema vijana ndio hulengwa zaidi na wanasiasa misimu ya siasa za uchaguzi mkuu kuwakabili wapinzani wao kwa manufaa yao ya kisiasa.
Lotuliang’iro sasa amewataka vijana kujitenga na wanasiasa ambao wanalenga kuwatumia visvyo na badala yake kujihusisha na maswala ambayo yatawanufaisha kimaisha.
Wakati uo huo Lotuliang’iro amewataka vijana kujitenga na matumizi ya mihadarati pamoja na pombe swala analosema linachangia vijana kujihusisha na maswala ya utovu wa nidhamu.