VIJANA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI.
Wito umetolewa kwa vijana katika kaunti hii ya Pokot magharibi kudumisha amani msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya na kutojihusisha na maswala ambayo huenda yakasababisha utovu wa usalama.
Ni wito wake kiongozi wa vijana youth Bunge katika kaunti hii Richard Todosia ambaye amewataka vijana na wakazi kwa jumla kufahamu umuhimu wa msimu huu na kutokubali kutumika na watu wenye malengo tofauti na kusababisha uvunjaji wa sheria.
Wakatio uo huo Todosia amewataka wadau kutumia msimu huu kuwashauri vijana kuhusu hali ya maisha na kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua vurugu hasa wakati huu ambapo taifa linakaribia siasa za uchaguzi wa mwaka ujao.