VIJANA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI.
Kiongozi wa vijana youth bunge katika kaunti hii ya Pokot magharibi Richard Todosia amewataka vijana katika kaunti hii kudumisha amani kabla wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti na kutokubali kutumika kusababisha vurugu katika mikutano ya wanasiasa.
Todosia ambaye pia ni mgombea kiti cha mwakilishi wadi ya mnagei aidsha amewataka wagombea viti vya kisiasa kuendesha kampeni zao kwa njia ya amani ili kuhakikisha kuwa utulivu unashuhudiwa katika kaunti hii na kuwapa wakazi nafasi ya kujitokeza kushiriki uchaguzi wa agosti 9.
Ni kauili ambayo imesisitizwa na baadhi ya vijana katika kaunti hii wakiapa kutotumika na viongozi wa kisiasa kuvuruga amani kwa manufaa yao ya binafsi.