VIJANA KWENYE KAUNTI YA UASIN GISHU WASHAURIWA KUTOTUMIWA NA WANASIASA KUVURUGA AMANI NCHINI


Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amewataka vijana kutotumiwa na wanasiasa ili kuzua vurugu kwenye hafla ya kisiasa wakati na baada ya uchaguzi mkuu.
Akizungumza na wanahabari mjini Eldoret, Mandago hata hivyo amewasuta wanasiasa ambao wameoneka kutumia vijana ili kuzua vurugu za aina yoyote.
Wakati uo huo viongozi wa kidini wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri wa dini ya kiislamu kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa Sheikh Abubakar Bini wameitaka tume ya uiano na utangamano wa kitaifa NCIC kuwajibisha viongozi wote ambao wanatoa matamshi ya uchochezi.