VIJANA KAUNTI YA POKOT WAHIMIZWA KUJISAJILI KUWA WAPIGA KURA


Naibu wa Spika katika Bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi Francis Krop ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kujitokeza kwa wingi katika usajili wa wapiga kura ambao umefikia siku yake ya tatu sasa.
Francis amesema huu ni muda mwafaka wa kubadilisha kituo cha kupigia kura kwa manufaa ya mpigaji kura mwenyewe.
Amesema kaunti ya Pokot Magharibi kila mara huwa na idadi ndogo ya watu wanaojisajili kupiga kura kutokana changamoto za ukame ambapo wafugaji huhamahama kutafuta maji na malisho katika taifa jirani la Uganda na kuwalazimu kukosa zoezi la kujisajili.
Hata hivyo amewahimiza kutafuta mbinu ya kufanikisha usajili na upigaji kura ikiwa ni njia mojawapo ya kupata viongozi wanaofaa.
Wakati huo huo amewatahadharisha vijana dhidi ya kuchochewa na wanasiasa kujitosa kwenye uhalifu uchaguzi mkuu unapokaribia.