VIJANA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATISHIA KUISHTAKI SERIKALI KUU KWA MADAI YA KUENDESHA OPARESHENI KAPEDO BILA KUWAJALI WATU WASIO NA HATIA


Vijana katika Kaunti ya Pokot Magharibi wakiongozwa na mwanaharakati Dennis Kapchok maarufu Mulmulwas na mwakilishi maalum Ozil Kasheusheu wametishia kuishtaki serikali kuu kwa madai ya kuendesha oparesheni katika eneo la Kapedo bila kuwajali watu wasio na hatia.
Vijana hao wamesema maafisa wa polisi wamezikandamiza haki za raia na wanyama wa eneo hilo.
Mulmulwas amesema serikali inafaa kutumia mbinu tofauti katika kuwanasa wahalifu wanaolengwa badala ya kuivamia jamii nzima.
Mwanaharakati huyo aidha amesikitishwa na hali kwamba wanahabari na malori yanayobeba misaada kwa wakazi wa Tiaty wamezuiliwa dhidi ya kuingia katika eneo hilo akitaja hali hiyo kuwa ni hatari kwa watu ambao wameathirika kwenye oparesheni hiyo.