VIJANA BUNGOMA WAHIMIZWA KUWATUNZA WAZAZI WAO.


Vijana katika kaunti ya Bungoma wamehimizwa kutowatelekeza wazazi wao hasa katika umri wao wa uzeeni na badala yake kuchukua majukumu ya kuwatunza.
Wakizungumza katika wadi ya Matulo eneo bunge la Webuye magharibi katika shughuli ya kumjengea nyumba mjane mmoja, viongozi wa dini katika kaunti hiyo wakiongozwa na Alex Masika, wamesema kuwa wengi wa wazee hao wanapitia hali ngumu ya maisha kwa kutelekezwa na wanao.
Wakati uo huo masika amewahimiza viongozi wa dini katika kaunti hiyo kufanya mazoea ya kuwatembelea washirika wao ili kubaini hali yao ya maisha na kuwasaidia wale ambao hajiwezi katika jamii.