UVAMIZI WA AFISI ZA UDA TRANS NZOIA WASHUTUMIWA


Vijana katika kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kutokubali kutumika kisiasa na baadhi ya wanasiasa kaunti hiyo kwa kisingizio cha tofauti zao za kisiasa.
Ni wito wake mshauri mkuu wa kisiasa katika afisi ya naibu rais William Ruto Dkt Abraham Sing’oei siku chache tu baada ya baadhi ya vijana kuvamia afisi za chama cha uda tawi la trans nzoia.
Aidha Sing’oei amesema chama hicho kinachohusishwa na naibu rais kingali changa na ipo haja ya kupewa nafasi ya kuimarika.
Wakati uo huo Sing’oei ameshutumu afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa kwa kutotekeleza majukumu yake inavyostahili kisheria na badala yake kuruhusu miingilio ambayo inahujumu baadhi ya vyama nchini.

[wp_radio_player]