UTULIVU WAREJEA KOITILIAL, ELGEYO MARAKWET.


Utulivu umeanza kurejea kwenye eneo la koitilial kaunti ya Elgeyo marakwet baada ya watu wawili kuuliwa kwa kupigwa risasi na wavamizi huku wengine 7 wakijeruhiwa vibaya.
Kulingana na mshirikishi wa eneo la bonde la ufa mohammed maalim amesema kuwa maafisa zaidi wametumwa eneo hilo kuimarisha doria na kuwasaka wavamizi ambao wamebadilihsa mbinu na saa kuvaa sare za polisi.
Jumla ya bunduki tano zimerejeshwa kufuatia oparesheni kali ya kiusalama Maalimu akiwahakikshia wakazi kuwa usalama umeimarishwa na kushinikiza ushirikiano baina ya maafisa wa polisi na wananchi.
Wakati uo huo Maalim ametoa hakikisho kuwa mtihani wa kidato cha nne KCSE utaendelea bila vizingiti kwani maafisa zaidi wa 100 wa akiba wametumwa kulinda shule mbali mbali.
Kauli yake maalim inajiri huku viongozi wa kaunti hiyo ya Elgeyo marakwet wakiongozwa na mwakislihi wa kike Jane Chebaibai wakiendelea kuilaumu serikali kwa kushindwa kukabili swala la utovu wa usalama katika eneo la bonde la kerio huku watu wakiendelea kuuliwa na mifugo kuibwa.