UTOVU WA USALAMA WAAATHIRI KUFUNGULIWA SHULE CHESOGON


Shughuli za masomo zinaporejelewa kote nchini kwa muhula wa kwanza, taharuki ingali imetanda katika eneo la Chesegon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na Elgeyo Marakwet kufuatia hofu ya mashambulizi kutoka kwa wahalifu, huku shule zikisalia bila wanafunzi na walimu.
Naibu mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Chesegon Joshua Powon, amesema kuwa kwa siku ya pili sasa wanafunzi na walimu hawajafika shuleni wakihofia usalama wao akielezea hofu kuwa huenda hali hii ikaathiri masomo eneo hilo.
Powon sasa anaitaka idara ya usalama kuwatuma maafisa wa polisi kushika doria katika maeneo hayo ili kuwahakikishia walimu na wanafunzi usalama wao.