UTOVU WA USALAMA BARINGO WAATHIRI USAJILI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA.


Huenda utovu wa usalama katika kaunti ya Baringo ukaathiri hatma ya baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza baada yaw engine kulazimika kuyahama makazi yao.
Baadhi ya wanafunzi katika eneo la Mochongoi kaunti hiyo ya Baringo wamelazimika kuhamia kaunti zingine kutokana na utovu wa usalama.
Baadhi ya wazazi wakiongozwa na Richard Kimosop wamesema huenda watoto wao wakakosa kujiunga na shule za upili kutokana na utovu wa usalama Baringo ambao umeathiri hali ya maisha huku mifugo wanaowategemea kujikiku kimaisha wakiibwa na wezi wa mifugo.
Yanajiri haya huku waziri wa elimu prof. George Magoha akisisitiza kwamba hakuna mwanafunzi ambaye anastahili kuzuiwa kujiunga na shule ya upili kutokana na ukosefu wa karo.