UTEUZI WA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA RAILA WAENDELEA KUPONGEZWA.

Baada ya mgombea wa urais katika muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga kumuteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza, sherehe zilisheheni katika mji wa Kitale kina Mama wakisifia hatua ya kumuteua Karua kwenye nafasi hiyo.
Kina Mama wakiongozwa na kiongozi wa maendeleo ya wanawake Kaunti ya Trans Nzoia Jane Kaitano, wamesema tangu Kenya ipate uhuru hakujakuwa na mwanamke katika nafasi kama hiyo akiwataka kina Mama kumpigia kura Raila Odinga.
Ni matamshi yaliyopigwa jeki na mwanasiasa Miriam Kubai aliyesema Raila ameonyesha mfano bora kauli sawa na hiyo ikitolewa na Sekta ya Boda boda ikiongozwa na Abraham Wangila.