UTEPETEVU MIONGONI MWA IDARA ZA USALAMA WATAJWA KUCHANGIA UTOVU WA USALAMA MIPAKANI MWA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET.


Utovu wa usalama katika mipaka ya kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet umechangiwa pakubwa na utepetevu miongoni mwa wakuu wa usalama serikalini.
Haya ni kwa mujibu wa mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema kuwa licha ya wakazi wa maeneo ambayo yamekuwa yakishuhudia uvamizi wa mara kwa mara kutoa majina ya washukiwa wa visa hivi, hamna hatua ambayo imechukuliwa kufikia sasa.
Aidha Moroto amedai kuwepo mapendeleo katika kukabili utovu wa usalama eneo hilo kupitia kuajiriwa maafisa wa akiba NPR akitaka usawa katika swala hilo.
Wakati uo huo Moroto amewataka wanasiasa kuendesha kampeni zao kwa utulivu na kutosababisha hali ambayo huenda ikasababisha utovu wa utangamano miongoni mwa wakazi ili kuwapa wakati mwema wa kuwachagua viongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kwa njia ya amani.