UTENDAKAZI WA EUGENE WAMALWA WATETEWA NA VIONGOZI TRANS NZOIA.
Viongozi mbambali kutoka Kaunti ya Trans-Nzoia wamejitokeza na kutetea utendaji kati wa waziri wa Ugatuzi Eugine Wamalwa kufuatia shutuma kutoka kwa wabunge Dkt Chris Wamalwa na Robert Pukose wakisema amewatekelezea mengi wenyeji wa Kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Alwain Sasaia ambaye ametangaza kuwania kiti cha eneo bunge la Endebess mwaka wa 2022, viongozi hao wamesema wenyeji wa salama wamepata hati milki kwa hisani ya waziri wamalwa mbali na mradi wa maji wa Kiptogot na ule wa kunyunyizia maji mashamba eneo la Kobei.
Aidha Sasaia amekosoa utendakazi wa uongozi wa sasa akisema umekosa kuwakarabatia wenyeji eneo bunge hilo zima barabara licha ya kupokea zaidi ya shilingi Milioni thelethini na mbili kutoka kwa halmashauri ya ukarabati wa barabara nchini KERRA kila mwaka.