USHURU UNAOLIPWA NA WAHUDUMU WA BODA BODA POKOT MAGHARIBI KUPUNGUZWA KUANZIA SEPTEMBA MOSI.


Agizo la gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi John Lonyangapuo kupunguzwa ushuru wanaotozwa wahudumu wa boda boda kutoka shilingi 300 hadi 200 kila mwezi litaanza kutekelezwa kuanzia tarehe moja mwezi septemba mwaka huu.
Haya ni kulingana na mkurugenzi wa idara ya utozaji ushuru kaunti hii ya pokot magharibi Francis Tuliamuk ambaye ametoa wito kwa wahudumu hao kushirikiana na idara hiyo kwa kulipa ushuru kwa wakati ili kuimarisha uchumi wao pamoja na wa kaunti kwa ujumla.
Wakati uo huo Tuliamuk ametoa wito kwa wahudumu hao wa boda boda kuzingatia masharti ya wizara ya afya katika kukabili msambao wa virusi va corona na pia kuhakikisha wanapokea chanjo dhidi ya virusi hivyo ili kuhakikisha usalama wao na wa wateja wao.
Ikumbukwe gavana wa kaunti hii John lonyangapuo alitangaza kupunguzwa ushuru huo kutokana na ombi la wahudumu hao mwezi mmoja uliopita wakati akizindua sacco ya wahudumu wa boda boda katika uga wa michezo wa makutano.