USALAMA WA IMARISHWA KATIKA ENEO BUNGE LA POKOT MAGHARIBI MSIMU HUU WA KRISIMASI


Usalama katika kaunti ya Pokot Magharibi umeimarishwa msimu huu wa sherehe za Krismasi na mwaka mpya.
Akithibitisha haya Kamanda wa Polisi kaunti hii Julius Kyumbule amesema kuwa wameongeza Maafisa wa polisi ili kuzidisha doria hasa maeneo ya watu wengi kama vile Masoko, vituo vya Magari, Maduka ya jumla na hata maeneo ya Kuabudu.
Kyumbule amesema kuwa Idara ya Polisi kaunti hii itaendeleza doria hadi pale Wanafunzi watakaporejea shuleni mwakani.
Aidha kyumbule ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kushirikiana na maafisa wa Polisi katika juhudi za kuhakikisha usalama wao umedumishwa kwa kufuata masharti ya serikali hasa kutopatikana nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri.
Kyumbule amewaonya Wamiliki wa Vilabu ambao wanawafungia wateja wao katika Vyumba hivyo nyakati za usiku na kukiuka masharti ya serikali kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupokonywa leseni za kuhudumu.