USALAMA POKOT MAGHARIBI WAIMARIKA KUTOKANA NA MICHANGO YA MASHIRIKA YA KIJAMII.


Miradi ya kilimo inayoendelezwa na mashirika mbali mbali kaunti hii ya pokot magharibi imechagia pakubwa kupunguza visa vya utovu wa usalama kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza eneo la Turkwel mwakilishi wa naibu kamishina kaunti hii Eric Okacha ambaye amesema kuwa mizozo mingi kaunti hii huzungukia swala la mifugo na juhudi za mashirika haya kuwafadhili wakulima imechagia kupunguza mizozo hiyo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na wakazi wa eneo hilo ambao aidha wamesema kuwa mashirika hayo yamewapa nafasi za ajira vijana wengi ambao waliasi wizi wa mifugo hali ambayo imechangia pakubwa kupungua utovu wa usalama eneo hilo.