USAJILI WA PIGA KURA WAPYA WATAJWA KUWATENGA WANAOISHI NA ULEMAVU.

Na Benson Aswani
Watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametengwa pakubwa katika shughuli nzima ya kusajiliwa wapiga kura wapya ambayo imekuwa ikiendelezwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Haya ni kwa mujibu wa aliyekuwa mshirikishi wa walemavu katika kaunti hii Patrick Limakeu ambaye amesema kuwa walemavu walipata wakati mgumu kuvifikia vituo vya kusajiliwa wapiga kura kutokana na mipangilio duni ya tume ya IEBC hali iliyopelekea idadi ndogo mno ya waliosajiliwa.
Aidha Limakeu amelaumu IEBC kwa kutokuwa makini kuzingatia sheria za uwakilishi wa walemavu hasa katika mabunge ya kaunti ambapo licha yao kuwasilisha majina mawili ya waliopendekezwa kuwawakilisha bungeni mwaka 2017 hamna aliyechaguliwa.
Hata hivyo afisa wa usajili katika eneo bunge la Pokot kusini Juma Mungwanga amesema kuwa waliendesha uhamasisho kwa walemavu kuhusu maeneo wanakopatikana japo akikiri kuwa hawakuweza kufikia idadi kubwa ya watu hao kutokana na uchache wa vifaa.