USAFIRI ENEO LA CHEPKOKOGH ENEO BUNGE LA SIGOR UNAZIDI KUIMARISHWA NA SHIRIKA MOJA LISILOKUWA LA SERIKALI


Shirika moja liso la serikali la UNDP linaendeleza ujenzi wa miundo msingi ikiwemo barabara eneo la chepkokogh katika kaunti hii ya Pokot magharibi, baadhi ya watawala wa eneo hilo wakipongeza juhudi hizo wanazosema kuwa zitarahisisha pakubwa shughuli za uchukuzi ambazo zimekuwa tatizo kutokana na kero la barabara mbovu.
Akiongea katika mkutano uliohusisha viongozi kutoka lokesheni ya chepkokogh wadi ya lomut chifu wa chepkokogh joseph kasiltich ameshukuru shirika lisilo la kiserikali la UNDP kwa kuwatengenezea barabara kutoka lomut hadi kamukekal jambo ambalo amesema kuwa litarahisisha usafiri katika eneo hilo.
Aidha chifu huyo ameomba wadhamini hawa kuwasaidia kumalizia barabara hiyo hadi chemustyo mpaka wa pokot na marakwet ili kurahisisha usafiri katika eneo hilo
Wakati uo huo mtawala huyo amekashifu kitendo ambacho jami ya pokot na marakwet wanazozania kisichojulikana kila mara wakisema hali hii imesababisha maafa ya kila mara.