UPOTOVU WA MAADILI MIONGONI MWA VIJANA

BUNGOMA


Shutuma zinaendelea kutolewa kwa kisa ambapo vijana ishirini na mmoja walipatikana katika mkahawa mmoja mjini webuye wakijiburudisha kwa vileo licha ya kuwa na umri mdogo.
Viongozi wa hivi punde ni naibu afisa msimamizi wa wafanyikazi katika serkali ya kaunty ya bungoma job chelongo ambaye alisema ni kitendo kibaya ambacho kitahujumu elimu ya watoto hao.
Aidha amewataka wazazi kuwa wangalifu na wanao hasa msimu huu wakiwa nyumbani ili mwasije wakapotoka kimaadili.
Hata hivyo ametaka hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mmiliki wa mkahawa na hata stakabadhi zake za biashara kupokonywa.