UPANZI WA MITI KATIKATI YA MJI WA KITALE WAZINDULIWA

Shirika moja la Kimazingira Kaunti ya Trans-Nzoia kwa jina kipsaina cranes and wetlands conservation Group  wakishirikiana na vijana wa kazi mtaani wamezindua kampeni ya upanzi wa miti  katikati mwa mji wa Kitale kama njia moja wapo ya kung’arisha na kuboresha  mazingara mjini humo.

Kwenye mkao na wanahabari baada ya shughuli hiyo Mwanzilishi  wa shirika hilo la mazingira  Maurice wanjala Sitoko amesema amechukua hatua hiyo kama himizo kwa vijana kukumbatia utunzaji wa mazingira mbali na kurembesha mji wa Kitale.

Aidha Wanjala ameongeza kuwa Mji wa Kitale unatazamiwa kuwa kitovu cha kibiashara kwa mataifa ya Uganda na Sudan kusini kutokana na uboreshwaji wa miundo msingi ya barabara unaoendelea  kwa sasa, akisema ipo haja ya kuimarishwa sura na kubadili hadhi ya mji wa Kitale kupitia kwa upanzi wa miti ilikuwa  kivutio kwa wageni na  wahekezaji zaidi.