UONGOZI WA TRANS NZOIA WAHIMIZWA KURAHISISHA SHUGHULI YA UTOAJI VITAMBULISHO.


Shinikizo zinazidi kutolewa kwa uongozi wa Kaunti ya Trans Nzoia kurahisisha shughuli ya utoaji wa vitambulisho kwa vijana waliohitimu kupata vitambulisho eneo bunge la Endebess badala ya kuwahangaisha kwa misingi ya kutoka mipakani.
Wakiongozwa na Paul Moiben vijana eneo hilo wametaka shughuli hiyo kurahishishwa ili kuruhusu vijana hao kupata stakabadhi hiyo muhimu itakayowasaidia kujisimamia na hata kushiriki katika kuwachagua viongozi wanaotaka mbali na kuendesha maisha yao.
Aidha Moiben amekariri kuwa uongozi wa miaka 10 wa serikali ya Gavana Patrick Khaemba haujazingatia usawa wa uwakilishi kwa wenyeji wa eneo la Endebes akitaka uongozi unaokuja kuhakikisha wenyeji eneo hilo wanajumuishwa kwenye maswala muhimu ya uongozi wa serikali ya Kaunti.