UONGOZI WA SHULE YA UPILI YA HOLY ROSARY WALALAMIKIA KUKITHIRI VISA VYA AJALI ZA BARABARANI ENEO HILO.


Wito umetolewa kwa idara inayohusika na maswala ya barabara kujenga matuta kwenye barabara karibu na shule ya upili ya wasichana ya holy Rosari kaunti hii ya Pokot magharibi.
Ni wito ambao umetolewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Consolata Sortun ambaye amesema kuwa ajali nyingi zimetokea eneo hilo kutokana na magari kuendeshwa kwa mwendo wa kasi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa waathiriwa wa ajali hizo.
Sortun ametoa wito kwa madereva wa magari pamoja na wahudumu wa pikipiki ambao wanatumia barabara hiyo kuwa makini wanapopita eneo hilo ili kuzuia ajali, huku pia akilaumu kutopata mafunzo maalum hasa kwa wahudumu wa boda boda.