UONGOZI WA KHAEMBA WAKOSOLEWA TRANS NZOIA.

Viongozi mbali mbali hasa wanaoegemea chama cha DAP-K katika kaunti ya Trans nzoia wameendeleza shutuma zao kwa uongozi wa gavana Patrick Khaemba kutokana na kile wamedai kushindwa kuwajibikia maswala ambayo yanawakumba wakazi wa kaunti hiyo.
Wakiongozwa na mgombea ugavana katika kaunti hiyo George Natembeya, viongozi hao wamemsuta gavana Khaemba kwa kutelekeza pakubwa sekta ya afya ambapo wakazi wanalazimika kutafuta matibabu katika kaunti zingine kutokana na huduma duni katika kaunti hiyo.
Aidha Natembeya amemsuta Khaemba kwa kutozingatia usawa katika utoaji wa fedha za basari ambapo wanafunzi kutoka jamii masikini wamekosa kunufaika na fedha hizo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwakilishi wadi ya kinyoro Lawrence Mogosu ambaye amedai kuwa serikali ya gavana Khaemba imefeli kutekeleza miradi ya maendeleo ya kuwanufaisha wakazi katika kipindi chake cha mihula miwili ambayo amehudumu kama gavana kaunti hiyo.