UONGOZI WA GAVANA LONYANGAPUO WAZIDI KUKOSOLEWA.


Uongozi wa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi umeendelea kukosolewa na viongozi mbali mbali kutoka kaunti hii miezi michache tu kabla ya kukamilika muhula wake wa kwanza ambao amehudumu kama gavana wa kaunti hii.
Akilinganisha muhula wake wakati akiwa gavana na gavana wa sasa, aliyekuwa gavana wa kwanza wa kaunti hii Simon kachapin amesema kuwa licha ya mgao mdogo ambao alitengewa katika kipindi chake, aliweka msingi bora wa maendeleo ikilinganishwa na utawala wa sasa licha ya kutengewa kiasi kikubwa cha mgao wa fedha.
Aidha Kachapin amelalamikia muda mrefu ambao tume ya kukabili ufisadi EACC inachukua kufanya uchunguzi kuhusu matumizi ya fedha katika serikali ya kaunti hii akidai fedha nyingi ikiwemo za basari zimefujwa na serikali ya gavana Lonyangapuo.
Kachapin sasa anatoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuwa makini katika uchaguzi mkuu ujao na kuwapiga msasa viongozi wanaotaka kugombea viti vya kisiasa ili kuwachagua viongozi kwa misingi ya utendakazi wao.