UONGOZI WA GAVANA LONYANGAPUO WAENDELEA KUSHUTUMIWA POKOT MAGHARIBI


Mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu ameendelea kukosoa uongozi wa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibvi John Lonyangapuo katika kipindi ambacho amekuwa madarakani.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki Kasheusheu amesema kuwa mbinu ya uongozi wa gavana Lonyangapuo imepelekea kuwa vigumu kufanya kazi na maafisa wengine katika serikali yake akiwemo aliyekuwa naibu wake Nicholas Atudonyang ambaye alijiuzulu baada ya muda mfupi wa kuhudumu.
Aidha Kasheusheu amepuuzilia mbali madai kuwa gavana Lonyangapuo amemsaidia kuimarika kisiasa baada ya kumteua kuwa mwakilishi wadi maalum kupitia chama cha KANU akisema kuwa Lonyangapuo alimpata akiwa tayari ameimarika kisiasa kufuatia ukosoaji wake wa serikali iliyotangulia.
Hata hivyo Kasheusheu amesema hamna tofauti za kibinsfi baina yake na gavana Lonyangapuo ila tu ni mitazamo tofauti ya kisiasa na jinsi mambo yanafaa kuendeshwa kaunti hii.