UONGOZI WA GAVANA LONYANGAPUO WAENDELEA KUKOSOLEWA


Seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi samwel poghisio ameendelea kukosoa hulka ya kubadilishwa kila mara maafisa wa serikali ya kaunti hii na gavana john lonyangapuo.
Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na kituo hiki, poghisio amesema kuwa hulka hii imetatiza pakubwa mipangilio ya serikali ya kaunti, akidai huenda gavana lonyangapuo ana nia fiche kutokana na mabadiliko hayo ya kila mara katika baraza lake la mawaziri.
Aidha seneta poghisio amendelea kulalamikia jinsi sekta ya afya inavyoendeshwa katika kaunti hii ya pokot magharibi hali ambayo imesababisha ukosefu wa dawa katika hospitali za kaunti hii, huku akimtaka gavana lonyangapuo kubadili mtindo wa utendakazi wake.
Wakati uo huo poghisio amekana madai ya kuwepo tofauti zozote za kibinafsi baina yake na gavana lonyangapuo akisema kuwa anatekeleza tu moja ya majukumu yake kama seneta wa kaunti hii, kuwajibisha uongozi wa kaunti katika sehemu ambazo anaona haziendi inavyopasa.
Ikumbukwe gavana lonyangapuo anatarajiwa kufika mbele ya bunge la seneti kuhojiwa kuhusiana na jinsi anavyosimamia kaunti hii.