UONGOZI ULIOTANGULIA WA LAUMIWA KWA KUTOTEKELEZA MIUNDO MSINGI POKOT MAGHARIBI

Mbunge wa Kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amelaumu uongozi uliotangulia maeneo anayoshuhudia ukosefu wa usalama hasa eneo la Tiati katika kaunti ya Baringo kwa kuchangia visa hivyo.

Akizungumza na wanahabari Moroto amesema kuwa viongozi wa eneo hilo walikuwa wakitekeleza miradi ya maendeleo kwa kulibagua eneo hilo huku akitoa wito kwa viongozi wa sasa kuhakikisha kwamba hali hiyo inarekebishwa.

Aidha Moroto amepuuzilia mbali shinikizo za kuendeshwa oparesheni ya kutafuta silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria akipinga pia madai kwamba utovu huo wa usalama unasababishwa na silaha kutoka taifa jirani la Uganda.

Kauli yake Moroto imetiliwa mkazo na baadhi ya viongozi wa kidini eneo hili ambao wamewataka viongozi kushirikiana na kanisa pamoja na wazee wa maeneo haya katika kuhakikisha kwamba utovu wa usalama unakabiliwa.