UNYANYAPAA WATAJWA KUWA KIZINGITI CHA HAKI KWA WAATHIRIWA WA HIV WALIODHULUMIWA KINGONO.

Wataalam wa afya, maafisa wa polisi pamoja na wale wa idara ya mahakama wametaja unyanyapaa na ubaguzi wa watu walioambukizwa virusi vya HIV kuwa kizingiti kikuu cha kupata haki kwa watu waliodhulumiwa kingono na kuambukizwa virusi hivyo.
Akiwahamasisha wadau mbali mbali kwenye warsha ambayo imefanywa na caps network program kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu na serikali ya kaunti ya Trans nzoia, mkurugenzi wa afya katika kaunti hiyo Nancy Kegode amesema asilimia kubwa ya waathiriwa hukosa kuwakilishwa na wakili na kuwa vigumu kwao kupata haki.
Naye afisa anayehusika na uhamasishaji wa HIV na maradhi ya ukimwi kwenye eneo bunge la Endebes Stephen Menjo amesema takriban watu 27 ni waathiriwa wa HIV huku visa vipya 700 vikiripotiwa kila mwaka katika kaunti.