UNYAKUZI WA ARDHI WAKITHIRI KABARNET, BARINGO.


Gavana Kaunti ya Baringo Stanley Kiptis amelalamikia visa vya unyakuzi wa ardhi ya umma ambavyo vimetekelezwa na watu binafsi na mabwenyenye hasa viungani mwa mji wa Kabarnet.
Akiongea wakati wa kuzindua bustani ya watu kujivinjari mjini Kabarnet gavana Kiptis amesema kuwa unyakuzi wa ardhi ya umma umeathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mji huo.
Gavana Kiptis ameongeza kuwa serikali yake imekua ikilazimika kununua ardhi licha ya kwamba ilikua ya umma ili kufanikisha miradi ya maendeleo kwani wanaotumuhiwa kunyakua ardhi hizo wana vyeti vya umiliki wa ardhi.
Aidha gavana Kiptis amewahimiza wakazi kuwa macho na kulinda ardhi yote ya umma dhidi ya unyakuzi kutoka kwa watu wachache.

[wp_radio_player]