UMUHIMU WA VYOO WASISITIZWA POKOT MAGHARIBI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuzingatia umuhimu wa kujenga vyoo katika maboma yao.
Akizungumza katika hafla ya kuangazia hatua ambazo zimepigwa katika kujenga vyoo eneo la Yualateke kwenye wadi ya Chepareria, waziri wa afya kaunti hii ya Pokot magharibi Christine Apakoreng amesema kuwa wakazi wataweza kuepuka magonjwa yanayotokana uchafu.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na msimamizi wa kitengo cha maji na usafi katika wizara ya afya Abel Koech ambaye amesema hatua hiyo itahakikisha usafi unadumishwa eneo hilo na kuepuka magonjwa mbali mbali.
Kwa upande wake mwakilishi wadi wa eneo hilo Patrick Lokomol amepongeza wadau wote waliofanikisha juhudi hizo.