UMILIKI WA ARDHI YA MUMBAI FARM TRANS NZOIA WAZIDI KUZUA UTATA WAKAZI WAKILILIA HAKI YAO.


Wanachama zaidi ya alfu moja washirika la Mumbai Farm wanaitaka serkali kuingilia kati na kuwapa maakazi kutokana na mahangaiko ya zaidi ya miaka 30 kupigania umiliki wa ardhi ya zaidi ya ekari alfu mbili kati yao na bwenyenye mmoja.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Harison Opanda na mwanachama Chege Ithaki wanasema bwenyenye huyo alikodesha Shamba hilo kwa miaka Ishirini baada ya Beberu alikuwa akifanyia kazi kurejea ulaya kuanzia mwaka wa alfu moja Miatisa Sabini na mbili.
Wanadai kuwa kwa muda huo wa miaka 20 bwenyenye huyo alikopa madeni chungu nzima kutoka kwa benki na mashirika mengine ya serikali akitumia cheti hicho cha kukodesha shamba deni lililomlemea kulipa na hivyo akaamua kuunda njama kununua shamba hilo lililokuwa limewekwa kwa mnada na serkali.
Wanasema hata hivyo bado hawajafurahia matunda la jasho lao kwani juhudi zao za kugawanya shamba zimelemazwa pakubwa na bwenyenye huyo.