UMASIKINI WATAJWA KUWA CHANZO KIKUU CHA WANAFUNZI WENGI KUKOSA KUHUDHURIA MASOMO POKOT MAGHARIBI.
Na Benson Aswani
Umasikini, njaa na ndoa nyingi zilizovunjika ndio maswala ambayo yamechangia pakubwa idadi kubwa ya watoto ambao hawaendi shuleni eneo bunge la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza siku chache tu baada ya kuzinduliwa oparesheni ya kuwarejesha watoto shuleni mkurugenzi wa elimu eneo hilo Edward Wangamati amesema kuwa jumla ya watoto elfu 22,800 hawajarejea shuleni kufikia sasa eneo la Pokot kaskazini, alfu 11,340 wakiwa wavulana huku alfu 11,460 wakiwa wasichana.
Wangamati amesema mipangilio ipo ya kuwahusisha wadau mbali mbali kuhakikisha mpango wa kuwarejesha watoto hao shuleni unafanikishwa huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatiwa mpango wa chakula shuleni, mpango anaosema utawasaidia wanafunzi wengi kutoka jamii masikini kusalia shuleni na kuendelea na masomo.