UKOSEFU WA MVUA WAIBUA HOFU KWA WAKULIMA TRANS NZOIA.


Viongozi kutoka kaunti ya Trans-nzoia wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa ukosefu wa mvua na uvamizi wa viwavi jeshi katika mashamba ya wakulima kaunti hiyo.
Wakiongozwa na mshauri mkuu wa kisheria katika afisi ya naibu wa rais Dkt Abraham Singoei, viongozi hao amesema hatua hiyo inatishia pakubwa utoshelezaji wa chakula mbali na kuongezeka kwa uhalifu na ufukara miongoni mwa wananchi wanaotegemea kilimo kwa mapato yao ya kila siku.
Aidha Dkt Singoei ametoa wito kwa serikali kuu na zile za kaunti kuingilia kati na kuwanusuru wakulima kutokana na viwavi jeshi ambavyo ni hatari kwa usalama wa chakula nchini,kwa kuwapa dawa bila malipo ili kuangamiza wadudu hao iwapo wanatarajia mavuno msimu huu.