UKOSEFU WA CHANJO MIONGONI MWA WATOTO

TRANS NZOIA


Ukosefu wa taarifu muhimu kuhusu chanjo, dhana potovu, uwoga wa kutafuta huduma hosipitalini kutokana na janga la corona na baadhi ya vituo vya afya kutumika kama vituo vya karantini katika kaunti ya transnzoia ni baadhi ya sababu zilizochangia akinamama kutowapeleka wanao kupata chanjo.
Afisa wa afya anayesimamia kitengo cha chanjo katika kaunti hiyo Angelina Otieno ni kwamba asilimia 14 ya watoto kwenye eneo hilo wako kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine wasipochanjwa.
Wakati wa kikao na wanahabari baada ya kukamilika kwa warsha iliowaleta pamoja washikadau mbalimbali wa sekta ya afya, afisawa mashirika ya Kenya AIDS CONSORTIUM na CANCO,Gregory Onyango anasema kwamba takriban watoo elfu 11 hawajapata chanjo.