UKOSEFU WA AJIRA WATAJWA KUWA CHANZO CHA UTOVU WA USALAMA BONDE LA KERIO.

Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wengi nchini umechangia wengi wao kujiingiza katika visa vya uhalifu ili kuweza kujikimu kimaisha na pia kumudu mahitaji ya familia zao.
Haya ni kulingana na ripoti ya utafiti kutoka shirika la kimataifa la international LAT ulioandaliwa katika kaunti ya Pokot magharibi, Turkana na Nairobi.
Afisa wa shirika hilo Fredrick Apoko amesema kwamba utafiti wao pia umebaini kwamba sekta ya kibinafsi ndio inayotoa nafasi nyingi za ajira kwa wakenya na hasa vijana.
Aidha Apoko amedai kwamba visa vya wizi wa mifugo vinavyoshuhudiwa kwenye baadhi ya kaunti nchini vinafadhiliwa na baadhi ya watu nchini wakiwamo wafanyabiashara wanaouza nyama.