UKEKETAJI WAPUNGUA SIGOR


Visa vya ukeketaji wa watoto wa kike eneo la Sigor kaunti hii ya Pokot magharibi vimepungua pakubwa hali ambayo imechangiwa na uhamasisho dhidi ya tamaduni hiyo ambayo inatolewa katika shule za eneo hilo.
Haya ni kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya ELCK Chesta Patricia Nandi ambaye amesema kuwa licha ya kuwa bado kuna vile ambavyo hufanywa kisiri, wanafunzi wengi wa kike wanafahamu madhara yake hali ambayo imewafanya wengi kutokubali kushiriki tamaduni hiyo.
Wakati uo huo Nandi ametoa wito kwa wazazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuwa makini na wanao na kutowaruhusu kushiriki baadhi ya tamaduni ambazo amesema huenda zikawapelekea kukosa kutimiza ndoto zao maishani.