UKEKETAJI NA NDOA ZA MAPEMA ZASALIA KIZUNGUMKUTI POKOT MAGHARIBI.
Licha ya juhudi za kukabili visa vya ukeketaji na ndoa za mapema katika kaunti hii ya Pokot magharibi imebainika visa hivi vingali kero miongoni mwa jamii.
Hii ni baada msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 kwa jina Lucy Cherop kulazimika kutembea kutoka eneo la alale hadi Kapenguria akitoroka kutoka ndoa aliyolazimishiwa baada ya kukeketwa.
Inaarifiwa mwathiriwa ambaye hajui waliko wazazi wake alikeketwa na mzee aliyeozwa kwake na jamii moja alikolelewa.
Hata hivyo aliokolewa na Msamaria mwema aliyepokea mjini makutano kaunti hii baada ya kutembea kwa zaidi ya kilomita 100 kutoka eneo la alale hadi Kapenguria huku wito ukitolewa kwa wanaoendeleza tamaduni hizo dhalimu kujitenga nazo ili kumpa mtoto wa kike fursa ya kuafikia ndoto yake maishani.